Heroe
From Wikipedia
Heroe | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
![]() Heroe wakubwa
|
||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
|
Heroe ni ndege wa jenasi Phoenicopterus, jenasi pekee ya familia Phoenicopteridae. Ndege hawa hukaa kwa maji ya chumvi kwa makundi makubwa. Wana miguu mirefu na shingo ndefu na nyembamba. Wakiruka angani hunyosha shingo. Urefu wao ni kati ya futi 3 na 5. Hula vijimea (algae) na nduvi ndogo ambazo huzikamata na domo lao zungu linalotumika kama chujio. Tago lao ni kifungu cha matope kwa tundu fupi ambalo ndani lake yai moja linatagwa.
[edit] Spishi za Afrika
- Phoenicopterus minor, Heroe Mdogo (Lesser Flamingo)
- Phoenicopterus roseus, Heroe Mkubwa (Greater Flamingo): anatokea Asia na Ulaya pia.
[edit] Spishi za Amerika
- Phoenicopterus andinus (Andean Flamingo)
- Phoenicopterus chilensis (Chilean Flamingo)
- Phoenicopterus jamesi (James's Flamingo)
- Phoenicopterus ruber (Caribbean Flamingo)