Managua
From Wikipedia
|
|
---|---|
Kanisa Kuu la Kikatoliki mjini Managua (Nikaragua) |
|
|
|
Mkoa | Eneo la mji mkuu Managua (Departmento Managua) |
Anwani ya kijiografia | Latitudo: 12°8′12″N - Longitudo: 86°15′5″W |
Kimo | 55 - 900 m juu ya UB |
Eneo | - Manisipaa 544 km² - mji 173.7 km² |
Wakazi | 1,380,100 (2001) |
Msongamano wa watu | watu 2,537 kwa km² |
Simu | +505 (nchi), 2 (mji) |
Mahali | |
Managua (Kinahuatl: Mana-ahuac - "kando la maji") ni mji mkuu wa Nikaragua pia mji mkubwa wa nchi hii mwenye wakazi milioni 1.3.
Mji uko kando la ziwa Managua unapoelea ufukoni kwa upana wa km 30 na kupanda mitelemko ya vilima hadi kimo cha mita 900.
Managua imekuwa mji mkuu tangu 1892[[1]] ilipochukua nafasi ya miji mikuu ya awali León na Granada.
Mji ulianzishwa katika karne ya 19. Iliharibika mara mbili na matetemeko ya ardhi (1931 na 1972) ikajengwa upya tena.
Managua ina vyuo vikuu kadhaa, vyuo na shule nyingi pamoja taasisi kama maktaba ya taifa na makumbusho ya taifa.
Makala hiyo kuhusu "Managua" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Managua kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |