Uruguay (mto)
From Wikipedia
Mto wa Uruguay | |
---|---|
|
|
Chanzo | milima ya Serra Geral (Brazil) |
Mdomo | Rio Plata |
Nchi | Brazil, Argentina, Uruguay |
Urefu | 1,790 km |
Kimo cha chanzo | takriban 1,800 m |
Mkondo | 4,622 m³/s |
Eneo la beseni | 370,000 km² |
Uruguay ni mto katika Amerika Kusini. Pamoja na mto Parana unaishia katika Rio de la Plata. Jina la Uruguay lamaanisha "mto wa ndege ya rangi nyingi".
Chanzo kiko katika Brazil ya Kusini kwenye jimbo la Santa Catarina. Mwanzoni mto ni mpaka kati ya majimbo ya Santa Catarina na Rio Grande do Sul ndani ya Brazil; baadaya mpaka kati ya Brazil na Argentina, halafu kati ya Argentina na Uruguay.
Jina la nchi Uruguay limetokana na mto. Asili ya jina la nchi ni "Jamhuri upande wa magharibi ya mto Uruguay".
Meli haziingii sana ndani ya Uruguay kutokana na maporomoko yake.
[edit] Viungo vya Nje
- Salto Grande Hydroelectric System (Kihisp.)
- Trivia about Uruguay (Kihisp.)
- From Uruguay Blog about everything uruguayan (Kiing.)