Auguste Beernaert
From Wikipedia
Auguste Marie Francois Beernaert (26 Julai, 1829 – 6 Oktoba, 1912) alikuwa mwanasheria na mwanasiasa kutoka nchi ya Ubelgiji. Kuanzia 1884 hadi 1894 alikuwa Waziri Mkuu na Waziri wa Fedha. Baadaye alikuwa mwakilishi wa Ubelgiji kwenye mikutano ya amani iliyofanyika katika mji wa The Hague mwaka wa 1899 na wa 1907. Mwaka wa 1909, pamoja na Paul d’Estournelles alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel kwa Amani.