Nadine Gordimer
From Wikipedia
Nadine Gordimer (amezaliwa 20 Novemba, 1923) ni mwandishi kutoka nchi ya Afrika Kusini. Hasa aliandika riwaya dhidi ya siasa ya ubaguzi ya rangi (yaani apartheid), na kuonyesha uharibifu katika maisha ya Waafrika. Mwaka wa 1991 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi.