Ufalme wa Byzantini
From Wikipedia
Ufalme wa Byzantini (Kigiriki: Βυζαντινή Αυτοκρατορία) ni neno linalotumika kuelezea Ufalme wa Roma uliozungumza Kigiriki katika Zama za Kati, ukiwa na makao yake makuu Constantinopo. Katika baadhi ya maana, hasa kuhususiana na wakati kabla ya kuanguka kwa ufalme wa Roma Magharibi, hujulikana pia kama Ufalme wa Roma Mashariki. Kwa wakazi wake, ufalme ulikuwa bado ni Ufalme wa Roma, na wafalme wake waliendeleza kurithiana mfululizo. Hata hivyo, kwa wakati mwingi wa historia yake, ulifahamika na wenzao wa magharibi kama “Ufalme wa Wagiriki” au “Ufalme wa Konstatinopo”, huku wenzao wa mashariki, ambao hawakurithi desturi za Kirumi, wakiendelea kutumia jina la ufalme la “Ufalme wa Roma”.