Afrika ya Mashariki ya Kijerumani
From Wikipedia
|
|||
Mwanzo wa utawala wa kikoloni | 1885 | ||
Makao ya serikali ya kikoloni | Bagamoyo hadi 1891 halafu Daressalam | ||
Eneo | 995.000 km² | ||
Wakazi | 7.700.000 (1913) | ||
Wakazi Wajerumani | 4100 (1913) | ||
Pesa | 1 Rupia= 64 Pesa, kuanzia 1905 1 Rupia = 100 Heller | ||
Nchi huru za leo | 1961 Tanganyika, tangu 1964 Tanzania Ruanda |
Afrika ya Mashariki ya Kijerumani (au: ya Kidachi) ilikuwa jina la koloni ya Ujerumani huko Afrika ya Mashariki kati ya 1885 hadi 1918/1919.
Eneo lake lilijumlisha nchi za kisasa za Tanzania bara (bila Zanzibar), Burundi na Rwanda. Ilikuwa koloni kubwa kabisa ya Dola la Ujerumani.
Koloni ilianzishwa na mfanyabiashara Mjerumani Karl Peters mwaka 1885 kwa niaba ya "Shirika la Kijerumani kwa Afrika ya Mashariki".
Baada ya upinzani wa wenyeji wa pwani mwaka 1889/1890 wakiongozwa na Abushiri na Bwana Heri serikali ya Ujerumani iliingilia kati na kufanya eneo lote kuwa koloni ya Dola la Ujerumani badala ya shirika.
Utawala wa Kijerumani ulikwisha katika Vita Kuu ya Dunia ya Kwanza (1914 - 1918) kutokana na uvamizi wa Uingereza na Ubelgiji.
Katika Mkataba wa Versailles mwaka 1919 eneo la koloni ya Kijerumani iligawiwa. Sehemu ya Tanganyika ilikabidhiwa kwa Uingereza na maeneo ya Rwanda na Burundi yaliwekwa chini ya Ubelgiji.