Andre Cournand
From Wikipedia
André Frédéric Cournand (24 Septemba, 1895 – 19 Februari, 1988) alikuwa daktari na mwanafiziolojia kutoka nchi ya Ufaransa; alihamia Marekani baadaye. Hasa alichunguza magonjwa ya moyo na tiba zake. Mwaka wa 1956, pamoja na Werner Forssmann na Dickinson Richards alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Tiba.