Atbara (mto)
From Wikipedia
Mto wa Atbara | |
---|---|
Chanzo | Ethiopia, milima ya Simien |
Mdomo | Nile kwenye mji wa Atbara (Sudan) |
Nchi | Ethiopia, Sudan |
Urefu | 800 km |
Kimo cha chanzo | m |
Mkondo | hubadilika sana na majira |
Eneo la beseni | 100,000 km² |
Atbara (Kiarabu: نهر عطبرة Nahr ʿAṭbara) ni tawimto wa Nile katika Ethiopia na Sudan.
Chanzo chake ni katika milima ya Simien (Ethiopia) takriban 50 km kaskazini ya Ziwa Tana au 30 km magharibi ya mji wa Gondar.
Tawimito yake ni hasa Tekeze na Setit. Kiasi cha maji ndani ya Atbara hubadilika sana. Miezi mingi ni mto mdogo sana unaopita katika nchi yabisi lakini wakati wa mvua katika nyanda za juu za Ethiopia inakuwa pana mwenye maji mengi.
Kwenye mji wa Atbara nchini Sudan inaishia katika mto wa Nile.
[edit] Viungo vya nje
- Maps of Ethiopia - Perry-Castañeda Library Map Collection, University of Texas