Basra
From Wikipedia
Basra (kar.: البصرة al-basra) ni mji kwenye kusini ya Irak mwenye wakazi zaidi ya milioni mbili.
Iko kando la Shatt-al-Arab inayopeleka maji ya Hidekeli na Frati hadi Ghuba ya Uajemi. Ni bandari kuu ya Irak.
Basra ni mji mkubwa wa tatu wa Irak baada ya Baghdad na Mosul. Wakazi karibu wote ni Waarabu na zaidi ya asilimia 90 Waislamu Washia.
Kama miji mingi ya nchi Basra imeathiriwa vibaya na vita ya Ghuba na mapigano yanayoendelea ndani ya Irak.