Bendera ya Zanzibar
From Wikipedia
Zanzibar ilhali ni sehemu ya Jamhuri ya Maungano ya Tanzania ilipata tena bendera ya pekee tangu Januari 2005. Inaunganisha bendera ya Tanzania na ile ya Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ya mwaka 1964 iliyotumika kati ya mapinduzi ya Januari na maungano ya Zanzibar na Tanganyika katika Juni 1964.
Zanzibar ilikuwa na bendera yake tangu kuhamia kwa Sultani wa Omani kutoka Maskat kuja Zanzibar. Bendera nyekundu ilikuwa sawa na ile ya Sharifa wa Maka.
Baada ya kupata uhuru mwaka 1963 usultani uliongeza alama ya karafuu katika bendera yake.