Carl na Gerty Cori
From Wikipedia
Carl Ferdinand Cori (5 Desemba 1896 – 20 Oktoba 1984) na Gerty Theresa Cori (15 Agosti 1896 – 26 Oktoba 1957) walikuwa wanakemia kutoka nchi ya Ucheki. Baada ya kufunga ndoa mwaka wa 1920, walihamia na kupata uraia wa Marekani 1922. Hasa walichunguza umetaboli wa kabohaidreti katika kiumbehai cha wanyama. Mwaka wa 1947, pamoja na Bernardo Houssay walikuwa washindi wa Tuzo ya Nobel ya Tiba.