Carola Kinasha
From Wikipedia
Carola Daniel Amri Kinasha ni mwanamuziki wa kike wa kitanzania. Alizaliwa Machi, 1970 huko Longido mkoani Arusha nchini Tanzania. Baada ya kumaliza masomo ya elimu ya msingi huko Longido, alihamia jijini Dar Es Salaam ambako alipata elimu ya sekondari na ya chuo kikuu. Carola amekuwa akijihusisha na masuala ya muziki tangu mwaka wa 1987. Ameshirikia katika miradi na matamasha mbalimbali ya kimuziki, ndani na nje ya Tanzania.