Chandrasekhara Raman
From Wikipedia
Chandrasekhara Venkata Raman (7 Novemba, 1888 – 21 Novemba, 1970) alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Uhindi. Hasa alichunguza mambo ya mwanga na jinsi unavyosambazwa kupitia vitu mbalimbali. Mwaka wa 1930 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia.