Dawit III
From Wikipedia
Dawit III (alifariki 18 Mei, 1721) alikuwa mfalme mkuu wa Uhabeshi kuanzia 8 Februari, 1716 hadi kifo chake. Alimfuata Yostos. Jina lake la kutawala lilikuwa Adbar Sagad. Chini ya utawala wake sinodi ya kanisa ilifanyika. Punde baada ya sinodi alifariki bila sababu kujulikana. Aliyemfuata kama mfalme ni Bakaffa.