Deutsche Welle
From Wikipedia
Redio Deutsche Welle (DW), au Sauti ya Ujerumani ni kituo cha Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani kwa ajili ya matangazo ya nje.
Kituo kimeanzishwa mw. 1953 kilitoa matangazo ya Kijerumani kwa ajili ya Wajerumani kote duniani kwa njia ya SW. Leo (2005) kituo hutangaza kwa redio za SM na FM kwa lugha 30 halafu kwa TV kwa lugha 4. Makao makuu ndipo Köln / Cologne; ofisi za DW-TV ziko Berlin.
Kwa www.dw-world.de [1] ratiba na matangazo hupatikana pia katika mtandao.
Ukurasa wa matangazo ya Kiswahili upo Sauti ya Ujerumani.