Frances Cabrini
From Wikipedia
Mama Frances Xavier Cabrini (15 Julai, 1850 – 22 Desemba, 1917) alikuwa mwanzishi wa jumuiya ya Masista Wamisionari wa Moyo Mtakatifu (kwa Kiingereza Missionary Sisters of the Sacred Heart). Jumuiya hiyo ilianza kufanya kazi hasa Marekani na kujenga shule, mahospitali na nyumba kwa watoto yatima. Mwaka wa 1946 Mama Cabrini alitangazwa kuwa mtakatifu akiwa Mmarekani wa kwanza kutangazwa hivyo. Sikukuu yake ni 22 Desemba.