Frank Kellogg
From Wikipedia
Frank Billings Kellogg (22 Desemba, 1856 – 21 Desemba, 1937) alikuwa mwanasiasa kutoka nchi ya Marekani. Kutoka 1925 hadi 1929 alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje. Hasa alijitahidi kutekeleza amani ya kimataifa. Mwaka wa 1929 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel kwa Amani.