George Gershwin
From Wikipedia
George Gershwin (26 Septemba, 1898 – 11 Julai, 1937) alikuwa mtungaji wa muziki kutoka nchi ya Marekani. Alitunga nyimbo nyingi zilizoathiriwa na mitindo ya Jazz. Pia alitunga opera moja iitwayo Porgy na Bess. Aliaga dunia mapema baada ya kupatwa na kansa ya ubongo.