Georgia (jimbo)
From Wikipedia
Georgia ni jimbo la kujitawala la Maungano ya Madola ya Amerika au Marekani. Iko katika kusini mashariki ya Marekani bara. Imepakana na Florida, Alabama, Tennessee, North Carolina na South Carolina. Upande wa kusini magharibii kuna pwani la Atlantiki.
Georgia ilikuwa kati ya koloni asilia 13 za Kiingereza katika Amerika ya Kaskazini zilizoasi dhidi ya Uingereza 1776 ikawa jimbo la Marekani 1788.
Jina la koloni asilia lilitolewa kwa heshima ya mfalme George II. wa Uingereza aliyekuwa pia mtemi wa Hannover.
Mji mkuu na mji mkubwa wa jimbo la Georgia ni Atlanta. Eneo la jimbo ni 154,077 km² na idadi ya wakazi inazidi milioni nane.
Takriban theluthi ya wakazi wana asili ya Kiafrika ni watoto wa watumwa wa kale.