James Rainwater
From Wikipedia
Leo James Rainwater (9 Desemba, 1917 – 31 Mei, 1986) alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Marekani. Hasa alichunguza nadharia ya atomu na kugundua mfumo isopacha wa kiini cha atomu. Mwaka wa 1975, pamoja na Aage Bohr na Ben Mottelson alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia.