Kamusi Hai ya Kiswahili Mtandaoni
From Wikipedia
Kamusi Hai ya Kiswahili Mtandaoni inajulikana kwa Kiingereza kama Internet Living Swahili Dictionary (kifupi: ILSD) inayoitwa pia "Kamusi Project".
Huu ni mradi wa Chuo Kikuu cha Yale (Marekani) hasa ya idara yake ya lugha za Kiafrika. Mradi huu unakusanya maneno ya Kiswahili pamoja na maana zao kwa Kiingereza. Unaongozwa na mwanzilishi na mhariri wake, Martin Benjamin.
Inapatikana kwa njia ya tovuti yake. Mtumiaji anaweza kuingiza neno lolote la Kiswahili au Kiingereza katika dirisha lake. Kama neneo lipo tayari kwenye kamusi atapata utafsiri wake katika maana mbalimbali.
Mradi ulikuwa na matatizo ya kifedha tangu mwanzo wa mwaka 2006 lakini umeweza kuanza upya kwa muda tangu Julai 2006. Mtu yeyote anayejiandikisha anakaribishwa kuchangia mle.