Karne
From Wikipedia
Karne ni miaka mia moja. Karne 10 ni milenia moja.
Neno limetokana na Kiarabu "ﻗﺮﻥ" linamaanisha kipindi cha miaka mia moja. Kwa kawaida karne si miaka 100 yoyote inayofuatana lakini kipindi kati ya miaka kama vile 1901-2000 au 1801-1900.
Karne inakwisha katika mwaka yenye "00" mwishoni yaani 1700, 1800, 1900, 2000. Sababu yake ni ya kwamba hakuna mwaka "0" ya kuanzisha hesabu hivyo karne ya kwanza ya hesabu ilianza kwa mwaka 1. Hali hii huleta kila karne majadiliano kwa sababu watu wengi husikia karne mpya inaanza wakati namba ya mbele waliyozoea muda mrefu inabadilika.
Hivyo watu wengi walisheherekea karne mpya mwanzoni wa mwaka 2000 iliyokuwa mwaka wa mwisho wa karne ya 20 si mwaka wa kwanza wa karne ya 21. Maoni ya wataalamu hayakueleweka au hayakupokelewa watu wengine walisema haidhuru.
Makala hiyo kuhusu "Karne" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Karne kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |