Kidaka
From Wikipedia

Kidaka ni sehemu ya mwambao wa bahari inayozungukwa na nchi kavu pande tatu. Ni kidogo kuliko ghuba na kwa kawaida pana kuliko hori iliyosababishwa na mdomo wa kijito au mto baharini na kuelekea ndani ya bara.
Kidaka mara nyingi ni mahali pazuri kwa ajili ya bandari asilia.