Talk:Kiswahili
From Wikipedia
Bold text
[edit] Idadi za Wasemaji wa Kiswahili
Ukurasa huu unasema eti kuna wasemaji wa lugha ya kwanza zaidi ya milioni ishirini na wasemaji wa lugha ya pili zaidi ya milioni sabini! Idadi hizi zinapatikana kweli? Sidhani. Ukiangalia makala haya kwa Kiingereza unapata milioni tano kwa wasemaji wa lugha ya kwanza na baina ya milioni thelathini na milioni hamsini kwa wasemaji wa lugha ya pili. Ukiwa na habari yo yote inayothibitisha hizi idadi, tafadhali tuambie! - 65.30.186.123 20:46, 16 Juni 2006 (UTC)
-
- Swali ni nzuri; wakati wa kutunga nilifuata ukurasa sujui upi. Nimejaribu kufuatilia swali lako na ugumu jinsi ilivyo mara nyingi ni ya kwamba makala kwenye mtandao ama hayataji marejeo au marejeo haya ni vitabu ambavyo haviwezi kusomwa kwa mtandao. Ninapenda kuonyesha ninachoona nipijaribu makadirio yangu hata kama mimi si mtaalamu.
-
-
- Kwenye kurasa ya majidiliano ya wikipedia ya Kiingereza swali linaulizwa pia na watungaji wanajibu: sina uhakika.
-
-
-
- Lugha ya kwanza: Nikijaribu kulinganisha yale yanayopatikana mtandaoni naona yafuatayo:
-
-
-
- Ukurasa wa wataalamu wa lugha wa ethnologue [[1]] wanataja idadi ndogo sana ya watu 772,642 wanaotumia Kiswahili kama lugha ya kwanza - ambayo mimi naona haifai kabisa.
-
-
-
- Hata kadirio ya milioni tano nahisi ni chini mno.
- Napiga kadirio langu: Tanzania wakazi milioni 38; nusu yao takriban chini ya miaka 18 yaani vijana milioni 19. Takriban 20% wakazi wa miji > watoto na vijana milioni 3,8. Ninahisi ya kwamba wengi sana kati yao watamjibu Mama kwa Kiswahili hata kama Mama anawaambia kitu kwa Kichagga, Kisukuma n.k. Asilimia ngapi? Sidhani ya kwamba mtu anajua kweli. 80-90%? Lakini mjini si vijana chini ya miaka 18 tu. Ningehisi hata idadi kubwa ya kikundi cha Watanzania mjini hadi umri wa miaka 30 hivi watafanya vilevile. Jumla yake hadi hapa 4-5 milioni? Hii ni bila watu wenye umri wa wastani mjini walioacha lugha za nyumbani na kuhamia Kiswahili. Tena wangapi?
- Nje ya mjini sina uhakika. Vijijini kabisa kuna maeneo ambako watu husema kilugha tu, sivyo? Lakini kuna pia vijiji hivi ambako makabila yamechanganya sana; hapo wageni wameanza kutumia lugha ya wenyeji; huko wenyeji wameanza kutumia lugha ya wageni, lakini kuna pia sehemu ambako wote wameshaanza kitambo kuwasiliana kwa Kiswahili hivyo sehemu ya watoto na vijana wamekua wakitumia Kiswahili hasa. Tukumbuke hata vijijini nusu ya wote ni chini ya miaka 18. Sasa wangapi wamehamia Kiswahili?? 10% au zaidi ya watu mashambani? Pale nilikoishi ningeona hata zaidi lakini siwezi kusema kitaifa. Basi niseme 10% - tena 3,8 milioni. Labda si wengi hivi.
- Kenya vipi? Asilimia ni ndogo kuliko Tanzania lakini mjini kote niliwasikia watoto wakisema zaidi Kiswahili kuliko lugha ambayo sielewi. Tuseme watoto na vijana milioni 3 walioko mjini - wangapi wanasema Kiswahili hasa? Labda robo? Pamoja na watu pwani nakadiria milioni 1 wasemaji wa Kiswahili ligha ya kwanza Kenya.
- Kongo ya mashariki na Uganda wa Kaskazini sijafika siwezi kusema.
- Kwa jumla: Hizi milioni 20 ni juu lazima tusahihishe. Milioni 5 za wiki ya Kiingerezea ni duni. Lazima tuseme "hakuna uhakika" - na nitaongeza: labda 8-10 Mil.
-
-
- Lugha ya pili:: yafuatayo ni kadirio langu. Kama mtu ana sababu ya kutaja asilimia tofauti ya wasemaji aseme tu!
-
-
Nchi Wakazi wote milioni % wasemaji wa Kiswahili kama lugha ya pili milioni Tanzania 38 95 36.1 Kenya 34 70 23.8 Uganda 28 30 8.4 Kongo 60 20 12 NCHI NNE -- -- 80,3
-
-
- Naona tutumia haya hadi mtaalamu wa kweli amepatikana. --Kipala 09:34, 17 Juni 2006 (UTC)