Kiwango utatu
From Wikipedia
Kiwango utatu ni kiwango cha maji au dutu nyingine inapoweza kuwa mahali pamoja katika hali imara, kiowevu na gesi (kwa mfano wa maji: barafu, majimaji na mvuke). Kiwango hiki kinategemea halijoto na shindikizo.
Kiwango utatu cha maji ni kiwango cha kukadiria skeli ya selsiasi au sentigredi (273.16 K au 0.01 °C).