Louis Renault
From Wikipedia
Louis Renault (21 Mei, 1843 – 8 Februari, 1918) alikuwa mwanasheria na mwelimishaji kutoka nchi ya Ufaransa. Alikuwa profesa wa sheria ya kimataifa na alijitahidi kama mpatanishi kati ya nchi mbalimbali. Mwaka wa 1907, pamoja na Ernesto Teodoro Moneta alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel kwa Amani.