Malabo
From Wikipedia
Malabo ni mji mkuu wa Guinea ya Ikweta mwenye wakazi 90,000 - 100,000. Iko mwambaoni wa Atlantiki kwenye pwani la kaskazini ya kisiwa cha Bioko (zamani: Fernando Po).
Mji ulianzishwa kwa jina la Port Clarence kuanzia 1827 na Waingereza waliokuwa wamekodi kisiwa cha Fernado Po kutoka kwa Hispania. Uingereza ulitumia kisiwa kama kituo cha jeshi la uanamaji lilizozunguka Atlantiki kwa shabaha ya kukomesha biashara ya watumwa. Waingereza walipeleka hapa watumwa waliopatikana kwenye meli za bishara ya watumwa. 1843 Waingereza walihamisha kituo chao ch kijeshi kwenda Sierre Leone na sehemu ya watumwa wa zamani waliopewa uhuru wao walibaki wengine wakafuatana na Waingereza kwenda Sierra Leone.
Wahispania walirudi polepole wakabadilisha jina la mji kuwa Santa Isabel.
Tangu uhuru wa Guinea ya Ikweta mwaka 1968 Santa Isabel ikawa mji mkuu. Wakati wa udikteta wa rais Francisco Macías Nguema jina lilibadilishwa kuwa Malabo. Idadi ya wakazi ilipungua sana kutokana na utawala wa kidikteta, wengi walikimbia kama wanachi kwa ujumla. Tangu mwisho wa Macias Nguema idadi imeongezeka tena lakini bado dalili ya uharibifu zinaonekana.
Pamoja na hasara hizo Malabo ni kitovu cha kiuchumi cha nchi. Mazao ya kakao, kahawa na ubao yanapelekwa hapa kwa meli na kuuzwa nje.