Martin Ryle
From Wikipedia
Martin Ryle (27 Septemba, 1918 – 14 Oktoba, 1984) alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Uingereza. Hasa alichunguza mionzi ya nyota na kuvumbua darubini inayotumia mawimbi na mwangi wa redio. Mwaka wa 1966 alipewa cheo cha Sir cha Uingereza. Mwaka wa 1974, pamoja na Antony Hewish alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia.