Mike Tyson
From Wikipedia
Michael Gerard Tyson (amezaliwa 30 Juni, 1966) ni mpiga ngumi wa uzito wa juu duniani unaotambuliwa na Shirikisho la Ngumi Duniani (WBC). Ni bondia wa kwanza kuwahi kutwaa taji hilo akiwa na umri mdogo. Mike alizaliwa katika mji wa Brooklyn New York. Alikuwa mtoto mtukutu akijihusisha na matukio ya uporaji mitaani. Alipelekwa katika shule ya kurekebisha tabia (Jela ya watoto) huko New York. Akiwa huko alionekana mwenye kipaji na mwalimu wa ngumi Mmarekani aitwaye Cus D'Amato ambaye matunda yake mengine ni mwanamasumbwi aitwaye Floyd Petterson na kutwaa taji la ngumi 1956.