Owen Chamberlain
From Wikipedia
Owen Chamberlain (10 Julai, 1920 – 28 Februari, 2006) ni mwanafizikia kutoka nchi ya Marekani. Hasa alifanya utafiti wa fizikia ya kiini na kugundua vipande vingi vya atomu. Mwaka wa 1959, pamoja na Emilio Segre alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia.