Rizavu
From Wikipedia
Rizavu ilikuwa eneo katika koloni za Uingereza ambako wazalendo waliruhusiwa kuishi kufuatana na mila na desturi zao. Katika mengi sheria zilizotawala maisha ya koloni zilikuwa sheria za Uingereza (pamoja na sheria za kimahali). Katika koloni zao Waingereza walipendelea muundo wa utawala kwa viongozi wazalendo kwenye ngazi za chini. Muundo huu ulitumiwa hata kwa maeneo makubwa katika nchi lindwa (protectorates) za uingereza.
Hasa katika koloni ambako Waingereza walitegemea kuongeza idadi ya walowezi Wazungu rizavu ilikuwa nchi ya pekee ambako wazalendo waliruhusiwa kuwa na mali ya ardhi.
Katika Afrika Kusini rizavu zilikuwa maeneo madogo yasiyo na rutba nzuri; ardhi yenye rutba nzuri ilidaiwa na walowezi au makaburu. Sheria ya ardhi ya Afrika Kusini iliweka asilimia tisa ya ardhi pekee kama rizavu. Baadaye wakati wa siasa ya Apartheid eneo hili lilipanushwa kidogo hadi 13% ya eneo la Afrika Kusini. Katika nchi hii rizavu zilibadilishwa kuwa Bantustan zilizopangwa kuwa nyumbani kwa mamilioni ya Waafrika weusi na mahali pa pekee ambako katika nadharia ya Apartheid walipangiwa haki za kisiasa.
Katika koloni kadhaa eneo al rizavu ilikuwa na asilimia kubwa zaidi kuliko Afrika Kusini lakini kwa jumla ardhi ya rizavu ilikuwa ndogo mno kwa mfano katika Kenya.
Uchumi wa kikoloni ulitegemea kazi ya wazalendo hivyo rizavu ilikuwa mahali pa kukalia kwa wakina mama, watoto na wazee wakati wanaume wengi walikaa nje na kuwafanyia kazi wenye mashamba ili wapate pesa ya kulipia kodi za serikali na mahitaji mengine. Haki ya kutunza mila na desturi ilitegemea masharti ya uchumi wa kikoloni. Mara nyingi kama sheria za wazalendo na sheria za kikoloni hazikupatana desturi ya wenyeji iliondolewa.
[edit] Linganisha
[edit] Marejeo ya Nje
- Kikuyu Colonial History - Rizavu kwa Wakikuyu wa Kenya
- Kamba Colonial History - Rizavu kwa Wakamba wa Kenya
Makala hiyo kuhusu "Rizavu" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Rizavu kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |