Rufiji (mto)
From Wikipedia
Rufiji ni mto mkubwa wa Tanzania. Chanzo iko Tanzania ya kusini-magharibi katika maungano ya tawimito ya Kilombero na Luwegu. Unafikia Bahari Hindi kwa njia ya delta yake takriban 200 km kusini ya Daresalaam karibu na kisiwa cha Mafia. Urefu wa Rufiji ni takriban 600 km.
Tawimto mkubwa katika beseni yake ni Ruaha Kuu.
Mwaka 2005 daraja lilikamilika linalorahisisha usafiri kati ya Daresalaam na mikoa ya Lindi na Mtwara.
[edit] Historia
Wataalamu kadhaa huamini ya kwamba mji wa kale ulioitwa Rhapta na kutajwa katika kitabu cha Periplus ya Bahari ya Eritrea ulikuwepo kwenye Delta ya Rufiji.
Wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia manowari ya Kijerumani SMS Königsberg ilizamishwa katika delta ya mto.