Shamu
From Wikipedia
Shamu (Kiar. شام "sham" - kifupi cha "bilad ash-sham" بلاد الشام ) ni jina kwa ajili ya eneo la kihistoria katika Mashariki ya Kati inayokaliwa leo hii na nchi za Syria, Lebanon, Palestina, Israel na Jordan.
Mipaka ya kijiografia ilikuwa mto Frati na milima ya Anatolia upande wa kaskazini, Bahari ya Mediteranea upande wa magharibi, Misri upande wa kusini na jangwa la Uarabuni upande wa mashariki.
Ni pia jina la kienyeji kwa ajili ya mji wa Dameski linalotumiwa mara nyingi nchini Syria.
![]() |
Makala hiyo kuhusu "Shamu" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Shamu kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |