Shebeli
From Wikipedia
Shebeli (pia: Shabelle, Scebelli, Shabell, Shebele) ni tawimto wa mto Juba inayobeba maji yake kutoka nyanda za juu za Ethiopia kuelekea Bahari ya Uhindi inagwa mara nyingi inakauka katika jangwa la Somalia kabla ya kufikia mdomo wake.
Chanzo cha Shebeli iko katika milima ya Batu (Ethiopia) takriban 200 km kusini ya Addis Ababa. Baada ya mwendo wa 920 km inaingia Somalia ikielekea Mogadishu. Karibu na mji unageukia kusini-magharibi na kufuata mstari wa pwani la Bahari Hindi kwa umbali wa 20-40 km ndani ya bara. Baada ya mwendo wa 900 km ndani ya Somalia lalio lake linaingia katika mto Juba lakini baada ya Mogadishu Shebeli ni kavu kwa sehemu kubwa ya maka.