Shmuel Yosef Agnon
From Wikipedia
Shmuel Yosef Agnon (17 Julai, 1888 – 17 Februari, 1970), au שמואל יוסף עגנון kwa Kiebrania, alikuwa mwandishi kutoka nchi ya Israel. Alizaliwa nchini Poland na jina la Shmuel Yosef Halevi Czaczkes. Akiwa bado kijana alihamia Israel. Hasa aliandika riwaya, na lugha zake zilikuwa Kiebrania na KiYiddish. Mwaka wa 1966, pamoja na Nelly Sachs alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi.