Tekle Giyorgis II
From Wikipedia
Tekle Giyorgis II (alifariki 1872) alikuwa mfalme mkuu wa Uhabeshi kuanzia 11 Juni, 1868 hadi 11 Julai, 1871. Alimfuata Tewodros II. Jina lake la kubatizwa lilikuwa Wagshum Gobeze. Kwa vile alikuwa mrithi wa nasaba ya Zagwe (upande wa baba yake) na mama yake alikuwa binti wa nasaba ya Solomoni, alijitangaza mfalme mkuu baada ya kifo chake Tewodros II. Utawala wake ulikuwa mfupi tu. Alishindwa katika mapigano na kukamatwa na Dejazmach Kassa aliyemfuata kama mfalme chini ya jina la Yohannes IV. Tekle Giyorgis II alifariki kifungoni baada ya mwaka mmoja tu.