TUKI
From Wikipedia
TUKI ni kifupi cha "Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili" ambayo ni idara ya Chuo Kikuu cha Daressalaam, Tanzania. Taasisi hii ni miongoni mwa taasisi kongwe za lugha nchini Tanzania. Madhumuni yake yakiwa ni kusimamia usanifishaji na maendeleo ya lugha ya Kiswahili.
Contents |
[edit] Historia yake
Ilianzishwa mnamo mwaka 1930 kama Kamati ya lugha (Kiswahili) ya Nchi za Afrika ya Mashariki, baadaye ikaitwa Kamati ya Kiswahili ya Afrika Mashariki. Mnamo mwaka 1964 kamati ilifanywa kuwa Sehemu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaamu. Baadaye ikaitwa Chuo cha Uchunguzi wa Lugha ya Kiswahili. Tangu 1970 kimepewa jina la Taasisi ya Uchunguzi wa Lugha ya Kiswahili.
[edit] Majukumu
Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili ni taasisi ya utafiti iliyopewa jukumu la kutafiti nyanja zote za lugha ya Kiswahili, fasihi na utamaduni, na kuchapisha matokeo ya utafiti huo. Hivyo pamoja na BAKITA (Baraza la Kiswahili Tanzania) TUKI ndiye mlinzi wa usanifu wa lugha ya Kiswahili katika Tanzania.
[edit] Kazi yake
Pamoja na kazi ya utafiti katika nyanja mbalimbali za Kiswahili, TUKI inatunga misaada ya kufundisha lugha na kamusi za Kiswahili mbalimbali. Kati ya kamusi hizi ni
- Kamusi ya Kiswahili sanifu,
- Kamusi ya Kiingereza -Kiswahili,
- Kamusi ya Kiswahili-Kiingereza,
- Kamusi Sanifu ya Isimu na Lugha,
- Kamusi Awali ya Sayansi na Tekinologia
- Kamusi ya Sheria
- Kamusi ya Biashara na Uchumi
TUKI imehariri toleo la Kiswahili la "Historia Kuu ya Afrika" iliyotungwa na kamati ya wataalamu ya UNESCO.