Wikimania 2006
From Wikipedia
Wikimania 2006 ni mkutano wa pili wa kila mwaka wa kimataifa wa Wikimedia. Mkutano wa kwanza, Wikimania 2005, ulifanyika mwaka jana nchini Ujerumani. Mkutano huu utafanyika Agosti 4-6 huko Cambridge, Massachussetts, Marekani. Wikimania ni mkutano wa kijamii na kisayansi ambao utajumuisha washiriki wa miradi ya Wikimedia ili kubadilishana mawazo, kujenga mahusiano, na kutoa taarifa za utafiti na juhudi mbalimbali za miradi hiyo.
Mkutano huu utatoa nafasi pia kwa washiriki wa miradi ya Wikimedia kukutana na kubadilishana mawazo na umma kuhusu miradi ya zana huria za teknolojia, maarifa huria na miradi ya wiki duniani.