Yesu Kristo.
From Wikipedia
Yesu Kristo (kutoka Kigiriki Ιησους Χριστός (Iesous Christos)) ni njia ya kawaida kati ya Wakristo jinsi anavyojulikana Yesu kutoka Nazareti (Yesu Mnazareti).
"Yesu Kristo" leo hutumika kama jina. Lakini kiasili ni tamko la imani lenye sehemu mbili: jina "Yesu" na cheo "Kristo". Kristo ni tafsiri ya neno la Kiebrania "mashiah" (Masiya). Katika lugha ya Kigiriki "Yesu Kristo" mara nyingi ni sentensi kamili. Maana yake kiasili ni "Yesu ndiye Masiya (mashiah)ya Mungu", yaani Yesu ndiye Masiya huyu aliyetangazwa na manabii wa kale anayesubiriwa na Israeli. Katika aya nyingine "Yesu Kristo" tayari imetumika kama jina. (linganisha: raisi Mkapa, au: Mkapa raisi - si yule Mkapa mwingine...)
Hata katika tafsiri ya Biblia hali hii bado inaonekana: wakati mwingine tunasoma "Kristo Yesu", wakati mwingine "Yesu Kristo", wakati mwingine "Yesu ni Kristo". Namna hii inaonyesha ya kwamba "Kristo" si jina tu; waandishi wa Biblia walielewa kabisa ni cheo.