Accra
From Wikipedia
Accra ni mji mkuu wa Ghana ikiwa na wakazi 1,970,400 (2005). Accra ni kitovu cha uchumi, biashara na mwasiliano ya nchi. Iko ndani ya mkoa wa Accra Kuu.
Accra ilianzishwa na Waga wakati wa karne ya 15 BK kama kituo cha biashara na Wareno. Wareno walijenga boma kwa ajili ya biashara hiyo na Wasweden, Waholanzi, Wafaransa, Waingereza na Wadenmark walifuata.
Eneo la Accra ya leo iliendelea kuwa mji kati ya boma tatu za Uingereza (Jamestown), Denmark (Osu) na Uholanzi (Ussherstown). Maeneo haya matatu leo ni kitovu cha mji wa kisasa.
Baada ya Waingereza kushinda Waashanti Accra ikawa mji mkuu wa koloni ya Pwani la dhahabu. Mji uliendelea kukua baada ya kujengwa kwa reli na bandari.
Accra ilikuwa pia mwanzo wa upinzani dhidi ya Waingereza ulioanzisha uhuru wa Ghana katika miaka ya 1940.
Leo hii Accra imepata mji wa kipacha wa karibu wa Tema baada ya kuhamishwa kwa viwanda na bandari kwenda Tema inayounganishwa na Accra yenyewe kwa reli na barabara kuu.
[edit] Viungo vya nje
- en: Accra Taxi Ride - video inayoonyesha safari ya Taxi katika Accra
- en: Mark Moxon, Travel Writer - Makala kuhusu ziara katika Accra mwaka 2002 (na picha)