Apia
From Wikipedia
Apia ni mji mkuu wa nchi ya visiwani ya Samoa katika Pasifiki mwenye wakazi 45,000. Iko upande wa kaskazini wa kisiwa cha Upolu.
Apia ni bandari kuu ya Samoa pia kitovu cha biashara na uchumi. Katika muda wa miaka 10 iliyopita biashara ilistawi vema mji ukakua. Kenye mtaa wa Vaitele kuna viwanda vya vipuli vya magari, nguo na vinywaji.
Mji umekua kando la mdomo wa mto Vaisigano penye kinga nzuri kwa meli. Kusini ya mji umepanda mlima Vaea (kimo cha 472 m).