Athi
From Wikipedia
Athi ni jina la mto katika Kenya, Afrika.
Mto wa Athi umeupatia jina lake kwa mji wa Athi River karibu na Nairobi pia kwa kampuni ya Athi River Mining.
Athi inaanza karibu na Nairobi ikielekea Bahari Hindi. Inapita Mbuga wa Wanyama wa Tsavo Mashariki pia tambarare ya juu ya Yatta ilipotafuta njia yake kuvuka eneo kubwa la mawe ya kivolkano.
Baada ya maporomoka ya Lugards Falls inapokea mto wa Tsavo ikibadilika jina lake. Mto unaitwa kuanzia hapa kwa jina la Galana. Kabla ya kufika katika Bara Hindi karibu na Malindi upande wa kaskazini jina limebadilika tena kuwa Sabaki.