Baeda Maryam I
From Wikipedia
Baeda Maryam (takriban 1448 – 19 Novemba, 1478) alikuwa mfalme mkuu wa Uhabeshi kuanzia 1468 hadi kifo chake. Alimfuata baba yake, Zara Yaqob. Wakati wa utawala wake alifaulu kupata maafikiano ya amani na Muhammad, mwana wa Badlay ibn Sa’ad ad-Din. Alifariki mahali pa Abasi Wera Gabayi. Aliyemfuata ni Eskender.