Bahri
From Wikipedia
Bahri au "Khartoum Bahri" (Kar: الخرطوم بحري al-Khartūm Bahrī = "Khartoum ya bahari yaani mtoni") ni mji wa Sudan jirani ya Khartoum upande wa kaskazini ya Nile ya buluu. Inaitwa pia "Khartoum ya kaskazini". Hata kama ni mji wa pekee kisheria halisi Bahri pamoja na miji ya Omdurman na Khartoum ni kama mji mmoja mkubwa sana unaounganishwa kwa madaraja kadhaa.
Bahri imekadiriwa kuwa na wakazi milioni 1.6 mwaka 2006.