Bangkok
From Wikipedia
Bangkok ni mji mkuu na pia mji mkubwa wa Uthai katika Asia Kusini-Magharibi. Kuna wakazi milioni saba walioandikishwa lakini imekadiriwa ya kwamba jumla ya wakazi inafikia hadi milioni 14-15.
Mji uko kwa 13°45′N 100°31′E kando la mto Chao Phraya karibu na mdomo wake katika Ghuba la Uthai.
Mji ulianzishwa kama bandari kwa ajili ya mji mkuuwa kale Ayutthaya. Mfalme Rama I aliyeanzisha utawala wa familia ya kifalme ya Chakkri alijenga jumba lake hapo mtoni na kuanzisha mji mkuu mahala pa leo.
Kuna mahekalu 400 ya Ubuddha mjini hasa Wat Phra Kaew.
![]() |
Makala hiyo kuhusu "Bangkok" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Bangkok kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |