Bern
From Wikipedia
Bern (pia: Berne, Berna) ni mji wa shirikisho wa Uswisi na mji mkubwa wa nne katika nchi. Bern ni pia mji mkuu wa jimbo la Bern. Iko kando la mto Aar. Hivyo ina nafasi ya mji mkuu ingawa shirikisho la Uswisi halina mji mkuu kikatiba.
Wakazi walio wengi hutumia lugha ya Kijerumani kwa lahaja ya Bern.
Mji uliundwa mwaka 1191 ukapokea jina kutokana jina la Kijerumani la dubu ("Bär").
Mkazi mashuhuri wa Bern alikuwa Mjerumani Albert Einstein aliyeunda nadharia zake za fizikia ya kisasa alipofanya kazi mjini Bern