Elihu Root
From Wikipedia
Elihu Root (15 Februari, 1845 – 7 Februari, 1937) alikuwa mwanasiasa kutoka nchi ya Marekani. Alikuwa mwanachama wa Chama cha Jamhuri cha Marekani. Kutoka 1905 hadi 1909 alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani. Mwaka wa 1912 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Amani.