Fritz Pregl
From Wikipedia
Fritz Pregl (3 Septemba, 1869 huko Laibach (leo Lubljana - Slovenia) - 13 Disemba, 1930 Graz – Austria) alikuwa mwanakemia kutoka nchi ya Austria. Aligundua mbinu za umikrokemia yaani uchambuzi wa kikemia penye kiasi cha dutu kidogo sana jinsi ilivyo mara nyingi katika uchambuzi wa sampuli za seli au viowevu vya kibinadamu kwenye maabara ya hospitali. Mwaka wa 1923 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia.