Heinrich Otto Wieland
From Wikipedia
Heinrich Otto Wieland (4 Juni, 1877 – 5 Agosti, 1957) alikuwa mwanakemia kutoka nchi ya Ujerumani. Alihariri kumbukumbu za kikemia za Justus von Liebig. Pia alichunguza mifumo ya kikemia ya sumu za uyoga na asidi ya nyongo. Mwaka wa 1927 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia.